A

A

Aliyetishia kumwua Obama, Netanyahu auawa na polisi akiiba kwenye benki Phoenix



Raia mmoja wa hapa jijini Phoenix, Arizona aliyeripoti kumwona mwanaume aliyevaa soksi ya kufunika kichwa na uso ispokuwa macho huku akiwa ameshika bastola na mfuko akitoka benki, aliwasaidia polisi kufika haraka na kumwua mwanaume mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Mario Edward Garnett (40) aliyekuwa anaondoka baada ya kuiba fedha.

Baada ya taarifa kufikia vyombo vya usalama, ndipo ikaelezwa kuwa Mario anahusishwa na matukio mengine ya 
wizi kwenye benki katika jiji la Atlanta, Georgia na jimboni Mississipi na kusababisha kifo cha polisi mmoja na kumjeruhi mwingine katika harakati za kutoroka asikamatwe baada ya kuiba.

Maosifa wa shirika la ujasusi la Marekani, FBI, liliweza kuoanisha matukio hayo kwa kuchunguza simu ya Mariao na kulinganisha na mwenendo wa matukio ya wizi wa benki alioufanya awali.

Mario wakati huo akiwa na miaka 30, mwajiriwa katika jeshi la polisi la Marekani aliyelifanyia kazi kwa miaka minne, aliwahi kufikishwa mahakamani na kukiri kutoa kauli ya vitisho kuwa angemwua rais, Barack Obama endapo angethubutu kuishambulia nchi ya Iran na kutoa vitisho vivyo hivyo kwa Waziri Mkuu, Bejamin Netanyahu na taifa lake la Israel: “If you order a strike on Iran, Im going to come up there and blow your brains out on national TV. You scheming hypocrite. You don’t mean anything to me. Youre just one dirt bag out of a handful plotting evil behind closed doors. Ive got plans for some of you, here shortly. … You scheming hypocrite ... Netanyahu is a dead man. Damn Israel. ... GOD has given Me a mandate. Glory belongs to GOD for all to come.”

Aliondoshwa jeshini na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miezi 8 jela (ambacho alikitumikia kwa mwezi mmoja tu kabla ya kuachiwa) ikiambatana na matibabu ya akili na kuwa chini ya uangalizi kwa miaka mitatu kwa kosa la kumtishia Rais wa nchi.

Inaelezwa Garnett aliyekuwa akiishi Oklahoma City, alikuwa na uhusiano na baadhi ya maafisa wa vyombo vya siri vya usalama ila haijaelezwa kwa kina kuhusu uhusiano huo.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako