Na Rashid Mkwinda — MKURUGENZI
Mstaafu wa iliyokuwa Radio Tanzania RTD Bw. Abdul Ngarawa amesema kuwa
weledi wa kazi za uandishi wa habari umeporomoka kutokana na baadhi ya
waandishi wa habari kutotumia vipaji vyao na badala yake kuiga sauti za
watangazaji wengine kwa kukosea.
Bw. Ngarawa amesema kuwa kazi ya uandishi na utangazaji mbali ya kuwa ni taaluma bali pia inahitaji kipaji cha mtu binafsi na kwamba waandishi wanaopenda kuiga sauti za watangazaji wa zamani wanakosea: ‘’Unapaswa kutangaza wewe kama wewe ili watu wakukubali wewe kama wewe uwe na utambulisho wako mwenyewe bila kuiga lahaja na sauti za wengine,’’anasema.
Alisema kuwa watangazaji wa sasa wanapaswa kujitahidi kutangaza kulingana kutokana na mazingira ya sasa kwa kujifunza zaidi na kufuatilia vyombo vingine vya habari kwa kufuatilia sera na maadili yao kwa nia ya kuboresha taaluma na weledi katika kazi ya Uandishi wa Habari na utangazaji.

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako