SAKATA LA ZITTO LAPELEKEA CHADEMA KUTANGAZA KUFANYA UCHAGUZI MKUU

Wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ikipinga waraka
uliosambazwa kwenye vyombo vya habari na katika mitandao mbalimbali sio
halisi, leo Chama hicho kimetangaza kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu
wa ndani, kuanzia balozi wa nyumba kumi hadi ngazi ya Mwenyekiti wa
Chama Kitaifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini
Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu amesema
kwamba mchakato wa uchaguzi huo utaanza rasmi Januari mwaka 2014 na
kukamilika Juni. Hatua ya CHADEMA kutangaza kuanza kwa uchaguzi huo ni
sawa na kujibu hoja iliyokuwa katika waraka uliosababisha Naibu Katibu
Mkuu wa Chama Zitto Kabwe na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Dk Kitilia
Mkumbo kuvuliwa nyadhifa zao zote ndani ya Chama.
Kwa muujibu wa waraka huo ambao Lissu amesema kwamba ni feki wahusika
walidai kwmaba lengo la kwanza ilikuwa ni kuandaa mpango mkakati wa
kuilazimisha Chama hicho kufanya Uchaguzi Mkuu kutokana na viongozi wake
kukwepa uchaguzi huo mara kwa mara.
Katika hatua nyingine
Zitto na Mwenzake Dk Kitilia wamepewa hati ya mashtaka ya tuhuma zao
yenye tuhuma 11 kila mmoja ambazo wanatakiwa kuyajibu kwa maandishi
ndani ya siku 14 kabla ya kuitwa katika Kamati Kuu kwa kujieleza kabla
ya maamuzi ya ama wafukuzwe ama wasifukuzwe kufanyika.
SAKATA LA ZITTO LAPELEKEA CHADEMA KUTANGAZA KUFANYA UCHAGUZI MKUU

Wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ikipinga waraka uliosambazwa kwenye vyombo vya habari na katika mitandao mbalimbali sio halisi, leo Chama hicho kimetangaza kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa ndani, kuanzia balozi wa nyumba kumi hadi ngazi ya Mwenyekiti wa Chama Kitaifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu amesema kwamba mchakato wa uchaguzi huo utaanza rasmi Januari mwaka 2014 na kukamilika Juni. Hatua ya CHADEMA kutangaza kuanza kwa uchaguzi huo ni sawa na kujibu hoja iliyokuwa katika waraka uliosababisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama Zitto Kabwe na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Dk Kitilia Mkumbo kuvuliwa nyadhifa zao zote ndani ya Chama.
Kwa muujibu wa waraka huo ambao Lissu amesema kwamba ni feki wahusika walidai kwmaba lengo la kwanza ilikuwa ni kuandaa mpango mkakati wa kuilazimisha Chama hicho kufanya Uchaguzi Mkuu kutokana na viongozi wake kukwepa uchaguzi huo mara kwa mara.
Katika hatua nyingine Zitto na Mwenzake Dk Kitilia wamepewa hati ya mashtaka ya tuhuma zao yenye tuhuma 11 kila mmoja ambazo wanatakiwa kuyajibu kwa maandishi ndani ya siku 14 kabla ya kuitwa katika Kamati Kuu kwa kujieleza kabla ya maamuzi ya ama wafukuzwe ama wasifukuzwe kufanyika.

No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako