A

A

Polisi Tanzania yamkamata Mnaigeria akiwa na mihadarati


Polisi wa Tanzania siku ya Jumamosi (tarehe 23 Novemba) walimtia mbaroni raia wa Naigeria anayeshukiwa kubeba kilogramu 30 za kokeni katika Uwanja wa Kimataia wa Kilimanjaro (KIA), gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti.

John Chizugo, mwenye umri wa miaka 29, alikuwa na mzigo huo ndani ya begi lake la kutembelea akielekea Roma kupitia Addis Ababa, kwa mujibu wa mkuu wa usalama wa KIA, Justine Kisusi. Inaaminika kuwa mtuhumiwa huyo alianza safari yake Arusha, Kisusi alisema.

Tukio hilo linakuja chini ya wiki moja tangu Waziri wa Usafirishaji Harrison Mwakyembe alipowataka maafisa wa usalama wa
KIA kuwa waangalifu kwa vile wasafirishaji wa madawa wamehamisha kambi yao kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

"Tumeziba nyufa zote kaitka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam," Mwakyembe alisema tarehe 19 Novemba, kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania. "Kwa hivyo ni jambo la kawaida kwamba wauzaji madawa kutumia KIA kama njia yao mbadala ya ndege ndani ya Tanzania."

Mwakyembe alilionya shirika la Maendeleo la Viwanja vya Ndege vya Kilimanjaro (KADCO) kwamba "mara ya pili ambapo suala lisilokubalika likitokea katika uwanja wa ndege, idadi ya watendaji kadhaa wa KIA watafukuzwa mara moja".

Mkurugenzi wa Fedha na Huduma Shirika wa KADCO Bakari Murusuri alisema kamba uwanja wa ndege umeunda kamati ya pamoja ya idara za polisi, usalama na uhamiaji, Mamlaka ya Usafirishaji wa Anga Tanzania (TCAA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, mashirika ya ndege, Mamlaka ya Mapato Tanzania na wadau wengine kuongeza usalama katika uwanja huo wa ndege. -- via Sabahi

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako