A

A

JE UNAFAHAMU HILI? HII NDIYO HIFADHI YA CHURA ANAEZAA‏, HAPATIKANI POPOTE DUNIANI ISIPOKUWA TANZANIA.

Wengi wanapenda sana kufahamu juu ya hifadhi ambayo kuna Chura pekee wanaozaa, na ambao hawapatikani sehemu nyengine lakini Tanzania Pekee.. hifadhi hii ni pekee kabisa inayo patikana katika korongo la la kihansi .. chura huyu wa Kihansi ni kama zilivyo raslimali nyengine na ni maliasili ya muhimu sana inayopatikana Tanzania
Chura huyu ambaye aligunduliwa mnamo mwaka 1996 katika maporomoko ya maji ya yaitwayo mahalala yanayopatikana ndani ya mlima Udzungwa wilayani kilombero mkoani Morogoro .Kwa hakika Chura huyu anaishi katika mazingira ya maji yanayo tiririka na kutoka kwenye mvuke wa kutosha unaotokana na nguvu za maji.
Pichani ni Bomba zilizowekwa na kutoa maji ya mvuke 'Sprinkers' kule kwenye korongo la Kihansi ambako ni makazi asilia ya chura kuwavutia chura kuishi kumejengwa na daraja la mbao kwa ajili ya kuvuka mto.
 
Chura huyu ambaye kwa ufupi na kwa jina lake la kingereza anaitwa Spray Toad na kwa jina la kitaalam anaitwa Nectophynoides asperginis ni moja ya kiumbe muhimu kwa sababu moja kubwa ya kuwa hapatikani katika sehemu yoyote duniani isipokuwa katika Bonde la kihansi Nchini tanzania  pekee..
 
Huyu ni Chura pekee katika jamii ya vyura wengi ambao mnawafahamu na waliopo duniani kwa sababu moja muhimu sana kuwa , chura huyu hutaga mayai na kukaa nayo katika kimfuko kilichopo ndani ya chura mwenyewe  hadi muda wa kuanguliwa unapotimia na ndipo huanguliwa na kutoa kiumbe kilicho hai. kwa Lugha nyepesi ni kwamba chura huyu huzaa kwa sababu  mayai anayotaga hayaonekani hubaki tumboni kwake hadi anapo zaa ndio watoto wanatoka nje.
 
Tabia hii muhimu ya vyura hawa kuzaa ndiyo ambayo inawafanya waendelee kuwa ni wapekee kabisa Duniani, tofauti na vyura wengine ambao wao hutaga na kuhifadhi mayai yao katika maji na mwishoe kuanguliwa. 

KWA KINA ZAIDI BOFYA HAPA
 

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako