Bifu ya Adam Juma na Nisher ,nani mchokozi ?
VIA VIBE MAGAZINE
Nani anakumbuka video ya ice cream ya noorah ? hii ndio
video iliyomtambulisha adam juma na visual lab kipindi hicho haijaenda
next level. adam juma ni nguli katika utengenezaji wa video na mhimili
mkubwa ambao sidhani kuna mtu anaweza kuja kuchukua nafasi yake.
ametengeeza mamia ya video za bongo kuanzai icecream , baridi kali ya
enika , mwana fa na lady jaydee hawajui , kuja kwa md dogg.kusema kweli
hauwezi kumaliza list ya video ambazo adam juma amefanya.
baada ya utawala wake kwa miaka yote hii ilipofika mwaka jana kuna
“chalii” mmoja wa arusha alianza naye kufanya videos.jamaa anajulikana
kama nisher. mshkaji alianza kufanya video fulani hivi za maunderground
na kama wewe sio mfuatiliaji mzuri wa videos za bongo unaweza kufikiri
kwamba video ya kwanza nsher kuifanya ikawa ni sijutii ya joh makini au
listen ya belle 9 , lakini siyo kweli. nisher alikua na video zake
nyingine ambazo zilikua hewani.
Baada ya nisher kukubalika sana na watu kwa kufanya video nzuri watu
wengi walianza kumpa sifa za kutosha na wengine kudiriki kumvua ufalme
wa video adam juma kitu ambacho kilizua utata. miezi saba iliyopita adam
juma aliamua kuvunja ukimya na kutupia comments zake kwa youtube katika
video ya mama yeyoo ya G.nako feat ben pol aliyoifanya nisher. adam
juma alimponda nisher kwa kutumia filters na effects .
kwa sasa adam juma ameacha kutengeneza music videos lakini jambo la
kushangaza ni picha aliyoipost nisher kwenye account zake za
twitter,facebook na instagram akiiponda kimafumbo kampuni ya visual lab
next level. nisher aliupload picha yenye maneno”i’m not next level, i’m a
new game”.
kitendo hiki kilimkasirisha adam juma na kufanya naye atoe yaliyo
moyoni kuhusu picha hii ya nisher. adam juma alizidi kumponda nisher
kutokana na kitendo hicho.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako