London, England
ARSENAL
imezidi kijichimbia kileleni mwa Ligi Kuu ya England, baada ya kuilaza
mabao 3-0 Cardiff City, kwenye Uwanja wa Cardiff jioni hii.
Mabao
ya Arsenal yamefungwa na Aaron Ramsey dakika ya 29 akimalizia pasi ya
Mesut Ozil na 90 pasi ya Theo Walcott na Mathieu Flamini dakika ya 86
pasi ya Ozil tena.
Ushindi
huo, unaifanya Arsenal itemize pointi 31 baada ya kucheza mechi 13,
ikiizidi Liverpool iliyo katika nafasi ya pili kwa pointi saba.
Katika mechi nyingine za Ligi Kuu England leo,
Everton
imeichapa 4-0 Stoke City Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, mabao
ya Gerard Deulofeu dakika ya 45, pasi ya Gareth Barry, Seamus Coleman
dakika ya 49 pasi ya Barry tena, Bryan Oviedo dakika ya 58, pasi ya
Gerard Deulofeu na Romelu Lukaku dakika ya 79 pasi ya Oviedo.
Bao
pekee la Gary Hooper dakika ya 30 limeipa Norwich ushindi wa 1-0 dhidi
ya Crystal Palace Uwanja wa Carrow Road, Norwich, Norfolk.
West
HamUnited imeifunga 3-0 Fulham Uwanja wa Boleyn Ground, London mabao ya
Mohamed Diame dakika ya 47, Carlton Michael Cole Okirie dakika ya 82 na
Joe Cole dakika ya 88.
Aston Villa imetoka
sare ya bila kufungana na Sunderland Uwanja wa Villa Park na mchezo wa
mwisho wa Ligi Kuu England, Newcastle United wataikaribisha West
Bromwich saa 5:30 usiku.
Ramsey hakutaka kushangilia baada ya kuifunga timu yake ya zamani |
Lukaku akishangilia bao lake leo |
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako