A

A

WAZIRI MKUU AAGIZA RANCHI ZA TAIFA ZIPITIWE UPYA NA WATANZANIA WAANZE KUNUFAIKA NA RANCHI HIZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh:Kassim Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye mkutano wa hadhara wilayani misenyi.Waziri Mkuu Mh;Kassim Majaliwa akiwa ameongozana na viongzo wa serikali kuelekea eneo la mpaka wa Tanzania na Uganda kaskanizini mwa wilaya ya misenyi.Waziri Mkuu na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi wakiangalia BICON ya mpaka kati ya Tanzania na Uganda wilayani misenyi.Waziri Mkuu akisoma ramani ya mpaka wa Tanzania na Uganda wakati alipotembelea ranchi ya Taifa iliyopo mpakani na Uganda.Kubwa alilokutana nalo Mh.Waziri Mkuu ni uingizwaji wa mifugo kiholela kutoka Uganda kuja Tanzania kutokana na mipaka kuwa karibu na makazi ya watu na vilevile kukosekana kwa ulinzi wa mara kwa mara.Waziri Mkuu akiwasili Kagera kuzungumza na wananchi.Katika mkutano huo,Waziri Mkuu ameagiza wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi kurudisha ranchi zote ambazo wawekezaji walipewa na wameshindwa kuziendeleza.Wakati huo huo Mwigulu Nchemba ametangaza kuanza kupitiwa upya kwa ranchi zote na blocks zake zianze kutumika kwa ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa wafugaji.Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akiwasili kwenye kiwanda cha uzalishaji wa sukari wilayani Misenyi,kiwanda cha KAGERA SUGAR.Baba wa Taifa Mwl.Julisu K.Nyerere alikizindua kiwanda hiki mwaka 1979 na baadae kikaja kuharibiwa wakati wa vita ya Uganda na Tanzania.Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa ubora wa miwa inayotumika kuzalishia sukari akitoa maelekezo kwa Mh:Waziri Mkuu Kassim Majaliwa namna uvunaji na uhifadhi wa miwa unavyofanyika katika kiwanda hiki cha Kagera.Uzalishaji wa sukari ukiendelea kwenye kiwanda cha Kagera Sugar,hii ni hatua ya mwisho ya kupakia sukari kwenye mifuko na kuihifadhi kwenye ghala.Hii ni sehemu ya stock ya sukari inayozalisha kiwandani hapo.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako