A

A

MWIGULU ATIKISA HAI,VUNJO,MWANGA NA ARUMERU KATA KWA KATA

Wananchi wa Hai Mjini wakimpokea Mwigulu Nchemba kwa shangwe.Mwigulu Nchemba ameshawasili Hai Mjini kuzungumza na Wananchi na Kumuombea Kura Rais Mtarajiwa kutoka Chama cha Mapinduzi Ndg,J.Pombe Magufuli.Mwigulu Nchemba akitoa Darasa kwa Wananchi wa Hai Mjini kuhusu Umuhimu wa Kuchagua kiongozi kwa Malengo,sio kuchagua Uongozi kwa Kishabiki."Wanahai naomba Mmchague Magufuli kwasababu ndiye kiongozi anayeweza kushughulika na Matatizo ya Wananchi wetu hasa swala la Rushwa,Uzembe maofisini na wadhurumaji.Kwa hapa Hai mmeshaonja ubaya wa Upinzani,hawajishughulishi kwa maendeleo Zaidi ya kupiga kelele zisizokuwa na tija kwa Wanahai".Wananchi wa Hai wakisema Nguvu Moja.Mwigulu Nchemba akiwasili USA river hapo jana.Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa USA River mapema hapo jana.Mbunge mtarajiwa wa Moshi Mjini Ndg.Davis Mosha akisalimiana na Mwigulu Nchemba wakati wa Mkutano wa hadhara ndani ya kata ya Sokoni.Mwigulu Nchemba akimnadi Davis Mosha mbunge Mtarajiwa kwa Moshi mjini.Mwigulu Nchemba akiwasili Same Mashariki.Mwigulu Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Same Mashariki Bi.Anna Kilango Malecela mapema hii leo wakati alipokwenda kuinadi Ilani ya CCM.Comrade Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Same Mashariki kuhusu Umuhimu wa kufanya Uchaguzi kwa Amani,Pia kuichagua CCM kwasababu imefanya kazi kubwa kuiletea Maendeleo Nchi yetu,Kwa Same serikali ya Magufuli nakwenda kujenga Barabara kwa kiwango cha Rami kuelekea Nkomanzi na Same Mashariki.Wananchi wa Mwigulu Nchemba akimndai Mathayo David Mgombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi.Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Vunjo kupitia CCM Ndg.Innocent Shirima hii leo.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Vunjo kuwa Mabadiliko sio vyama,Mabadiliko ni shughuli za maendeleo na Utendaji kazi.Magufuli anakwenda kubadilisha Utendaji kazi na Usimamizi wake.
Picha na Sanga R.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako