A

A

MWIGULU NCHEMBA AFUNIKA IRAMBA,HANA MPINZANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA WABUNGE

Mh.Mwigulu NChemba akipokea Fomu ya kuwania Ubunge kwa mara nyingine kwa Jimbo la Iramba,Mwigulu amechukua fomu hiyo hii leo Makao makuu ya CCM Wilaya ya Iramba-Kiomboi.Mwigulu Nchemba akisainii kitabu maalumu cha Wagombea Ubunge Jimbo la Iramba.Msafara MKubwa wa Mh.MWigulu Nchemba ukielekea Makao  Makuu ya CCM Wilaya ya Iramba kwaajili ya Kuchukua fomu ya Kuwania Ubunge kwa awamu ya pili.Mwigulu Nchemba akiwa ameungana na Vijana wa Bodaboda waliomiminika kumsindikiza akachukue fomu ya kuwania Ubunge kwa mara ya pili ndani ya Wilaya ya Iramba.Mwigulu Nchemba akiwasili Ofisi za chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iramba,Mamia ya Wananchi walijumuika naye kumsindikiza ili awezekuchukua Fomu hiyo na hatimaye kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuwa Mgombea Ubunge Wilaya ya Iramba.Mwigulu Nchemba akimtambulisha Mke wake Bi.Neema Mwigulu kwa Wananchi waliofika kushuhudia Mbunge wao akichukua fomu ya kuwania Ubunge kwa mara nyingine katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.Sehemu ya Mamia ya Wananchi waliofika ofisi ya CCM wilaya ya Iramba kushuhudia Uchukuaji wa Fomu wa mbunge wao Mh.Mwigulu Nchemba hii leo.Ni Mwigulu Nchemba tena 2015 ndani ya Wilaya ya Iramba akiwania Ubunge kwa awamu ya pili,Awamu ya kwanza akiwa ameandika Hostoria kadhaa katika uso wa maendeleo ya Jimbo la Iramba tangu Uhuru.
Mwigulu Nchema ambaye ni Mbunge wa Sita tangu Wilaya ya Iramba ianzishwe,amepokea Kijiti cha Ubunge Mwaka 2010 kutoka kwa Aliyekuwa Mbunge Ndugu.Kirimba.Mara baada ya kuchukua Ubunge wa Iramba ,Mwigulu Nchemba amebadilisha sura ya maendeleo ya Jimbo hilo katika maeneo ya Fuatayo.
Mwigulu Nchemba wakati akiingia kuwa Mbunge wa Iramba alikuta Wilaya inaumeme maeneo ya Tarafa tu,Kata na Vijiji vilikuwa havina Umeme.Hivi sasa Mwigulu Nchemba amefanikiwa kuwasha umeme katika kata zote na Vijiji 48 vya Jimbo Zima.Hii haikuwahi fanyika kabla ya Mwigulu kuwa Mbunge wa Iramba.
Mbali na Umeme,Mwigulu Nchemba akitambua shida ya Maji inayolikumba jimbo lake,Amefanikiwa kufungua miradi 8 ya Maji katika Kata ya Ndago,Shelui,Mgongo,Kyengege,KInapanda n.k Wakati huo vijiji Zaidi ya 62 hivi sasa visima vinachimbwa ilikufanikisha huduma kwa Wananchi wake.Pia ujenzi wa barabara za ndani ya Jimbo na hata za kuunganisha na wilaya zingine zimeimarishwa na hata kupandishwa daraja kuwa chini ya TANROADS.
Kwa maendeleo hayo na mengine kama Kusomesha watoto wa familia zisizojiweza Zaidi ya 200,Kusambaza vitabu kwa kila shule vyenye thamani ya Tsh.Milion 7 kwa kila shule.Pia amekwenda mbali zaidi amekuwa Mbunge wa Kwanza kusambaza dawati 200 kwa kila shule ya Jimbo lake na Mbunge pekee aliyechangia Mifuko zaidi ya 100 kwa kila shule kwaajili ya Ujenzi wa maabara pamoja na Flame zake za Madirisha na Milango.
Maendeleo yote haya ambayo hayakuwahi kufanywa na wabunge waliopita kunampatia nafasi kubwa sana Mwigulu Nchemba kuendelea kuwatumikia wananchi wa Iramba,Kwa Taasisi za Kidini amekuwa mstari wa mbele kujenda na Kufunika Makanisa na Misikiti mbalimbali ndani ya Jimbo lake.
Wananchi wa Iramba hii leo wamejumuika naye kuhakikisha anakamilisha hatua zote za ndani ya Chama na taratibu za Uchaguzi ili tar.25/10/2015 aweze kuchaguliwa tena kuwaongoza.
Mwigulu Nchemba anaandika historia ya pekee kuwa Mbunge wa Iramba mwaka 2010,Mwaka 2011 analiteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Mh;Jakaya Mrisho kikwete kuwa Mtunza hazina ya CCM Taifa,Mwaka 2012 Mwigulu anachaguliwa tena kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara ikiwa ndio mara ya kwanza CCM inakuwa na Kiongozi Mkubwa(Top 4) mwenye Umri chini ya miaka 40.
Mwaka 2013 Mwigulu Nchemba ameteuliwa kuwa Naibu Waziri  wa Fedha anayehudumia Sera.Mtiririko huu wa Uongozi na kwa kuzingatia namna alivyokuwa mstari wa mbele kusimamia maslahi ya Watanzania wote (wanyonge na Masikini) na hatiye kujitosa kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano.Mwigulu Nchemba anaonekana ni TAA mbele ya Wanairamba na hivyo wamekuwa wakisisitiza kuwa ndiye chaguo lao na Wanaimani naye kubwa kuwa atawasadia katika kupandisha shughuli za maendeleo yao.
Kauli mbiu ya Mwigulu iliyoshika kasi Nchini kwa sasa ni "MABADILIKO NI VITENDO NA WAKATI WAKE NI SASA"

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako