A

A

TASWIRA UFUNGUZI WA BARAZA LA PILI WA WATUMISHI WA TAASISI YA UHASIBU (TANZANIA INSTUTE OF ACCOUNTANCY)

Mkutano wa Raraza la pili la Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu likiendelea.
 Mwenyekiti wa Baraza la pili la
Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Ndugu,Jairo akifafanua kazi za Baraza hilo katika Vyuo vya uhasibu Nchini.Naibu Waziri wa Fedha(S) Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo,Kubwa amesisitiza mfumo mpya wa uajiri wa watumishi wa Umma ambao utakidhi mahitaji ya wahadhiri vyuoni na hata kwenye Taasisi zingine,Taasisi za Elimu na fedha zingepewa mamlaka ya kuajiri kutokana na uhitaji wao mara baada ya fungu la bajeti la kuajiri kupita,Hii itarahizisha ukiritimba wa kazi kwa mazoea na taasisi hizi kukosa watumishi wa kutosha kuhudumia idadi ya wanafunzi/wahitaji huduma.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo wakisikiliza hotuba ya Mh:Mwigulu Nchemba ambaye amewahakikishia kuwa Wizara ya fedha itaendelea kutoa na kuwekeza nguvu zake kwenye Taasisi za elimu hasa uhasibu kwaajili ya kuhakikisha vyuo vinatoa huduma stahiki.Prof.Kamzora Makamu wa Chuo kikuu cha Mzumbe akitoa shukrani kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwakuonesha njia kuwa Vijana wanaweza kufuta Utumishi wa Mazoea,tena katika swala la ajira.Profesa amesema Mwigulu anajibu wazi wazi mambo yote ambayo Mwl.Nyerere aliandika kwe ye Kitabu chake cha TUJISAHIHISHE"Sijawahi kusikia kiongozi nchi hii anaweza kuwa na maono kama yako tena ya kimabadiliko,Tumia maono haya kuifikisha Tanzania kwenye neema ambayo wengi wanapenda kuifikia"alisema Prof.Mh:Naibu waziri wa Fedha akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi /wajumbe wa Baraza la pili la Watumishi wa Taasisi za Uhasibu ambao hii leo Baraza lao limefunguliwa Rasmi na Mh:Mwigulu Nchemba.

Picha/Maelezo na Festo Sanga-Bagamoyo

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako