A

A

TANGA LEO,COMRADE MWIGULU NCHEMBA ATIKISA WILAYA ZAIDI YA 7 TANGA KWA SIKU MOJA

Hisia za Wananchi wa Korogwe zikiwa zimeandikwa kwenye Bango hili kama linavyosomeka,Hii imetokea Korogwe Mjini wakati Naibu katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya kutembelea wilaya zote za Mkoa wa Tanga hii leo.Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake aliyoifanya kwa siku moja(17.01.2014) kwa wilaya zote za Mkoa wa Tanga.Naibu katibu Mkuu akiwasili Viwanja vya Tangamano-Tanga Mjini hii leo kuzungumza na Wananchi wa Tanga,Kubwa amesisitiza wananchi kutijitokeza kupiga kura,kufuatilia mapato na matumizi ya Halmashauri zao.Pia amesisitiza kuwa Machinga wanaofanya kazi zao soko la Tangamano wasichukuliwe kama sehemu ya Uchafu,bali serikali iwawekee Utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao.Wananchi wakigombania angalau kusalimiana na Naibu katibu Mkuu alipowasili Muheza Tanga hii leoNaibu katibu MKuu akisalimiana na Wananchi wa Kilindi hii leoMkutano ukiendelea wilaya ya Kilindi.Naibu katibu Mkuu akizungumza na Wananchi wa Handeni hii leo wakati wa ziara yake ya Kuhamasisha wananchi kuendelea kuiunga mkono CCM,Pia kujitokeza kupiga kura.Wananchi wa Nkinga(Maramba)  Mkoani Tanga wakisalimiana na Mh:Mwigulu NchembaComrade Mwigulu Nchemba akiteta na Wananchi wa Handeni wakati alipofanya mkutano wa kuzungumzia utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi na Umuhimu wa kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura.Hisia za Wananchi kwa Naibu katibu mkuu zikiwa zimeandikwa kwenye mabango wilayani Handeni.Sehemu ya mamia ya Wananchi wakisikiliza Mkutano wa Naibu katibu Mkuu wilayani Korogwe.Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa korogwe Mjini.Hisia za Wananchi wa Korogwe kwa Mwigulu Nchemba,hii inatokana na utendaji kazi wake unaogusa watanzania waliowengi.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Korogwe Mjini kuhusu utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi hususani kwenye Miundo mbinu na shughuli za Kiuchumi."Kitapataje kibanda cha Uchohoroni DAWA ambazo Serikali haina???" Kuna watumishi wa serikali wanaiba dawa na kuwaelekeza wananchi kwenda Kuzinunua kwenye Maduka yao ya Dawa.Mwigulu Nchemba amesema wakati umefikwa kwa Watanzania kuwa walinzi wa mali za Umma,Kuchukua hatua kwa vitendo dhidi ya wakwamisha maendeleo.Picha imecgukuliwa Korogwe Mh:Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Korogwe Mjini mara baada ya Kuhitimisha ziara yake aliyoifanya kwa Mkoa wote wa Tanga kwa siku moja,Lengo likiwa kueleza kuhusu utekelezaji wa ilani ya  Chama cha Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako