A

A

MWANZA HII LEO,MKUTANO ULIOACHA GUMZO HUU HAPA

Mapokezi ya Mwigulu Mwanza jioni ya leo tar 12.12.2014 Viwanja vya shule ya Msingi Mabatini.Mwigulu Nchemba akiwasili Viwanja vya Mabatini akiwa amongozana na Mwenyekiti wa Geita Ndugu Joseph Msukuma.Wananchi wakifurahia Ujio wa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Comrade Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Mabatini Mwanza hii leo.Naibu katibu Mkuu CCM Bara akionekana kukasilika na Kitendo cha Machinga na Mamantile kunyanyaswa Jijini Mwanza,Hivi sasa ameomba Halmashauri ya jiji la Mwanza iangalie upya swala la Kufukuza Machinga kwasababu hakuna tija kuacha Matajiri wakwepe kodi halafu tukimbizane na Machinga.Sehemu ya Umati wa Wananchi wa Mabatini Mwanza wakimsikiliza Mwigulu Nchemba.Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Mwigulu Nchemba amewaomba wakazi wa Mwanza kufanya Mabadiliko kwa Vitendo sio Kubadilisha Vyama.Ameomba waunge mkono jitihada za Chama cha Mapinduzi na wajitokeze kuwapigia kura wagombea wa Chama cha Mapinduzi.Awali Mh:mwigulu Nchemba alifanya mkutano Uwanja wa Bwaloni Mwanza kabla ya Kueleka Mbatini,Hapa akizungumza na Wakazi wa Bwaloni Mwanza kuhamasisha Uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho kutwa.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako