A

A

Hiki ndicho kilichomfanya Annan aseme Ebola ni ugonjwa wa watu maskini.

Annan BetterMwana Diplomasia kutoka Ghana ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) Kofi Annan amesema ugonjwa wa Ebola ni wa ‘maskini’ na sio matajiri.
Annan amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha CNN ambapo amezungumzia sababu kadhaa zinazopelekea mapambano ya dhidi ya Ebola kuchukua muda mrefu huku maelfu ya watu wakipoteza maisha.
Katibu Mkuu huyo mstaafu amesema Ebola ni
ugonjwa wa maskini kwa kuwa tangu ugundulike ni takribani miaka 40 imepita, ambapo kwa nchi tajiri ingewezekana kufanyika tafiti ambazo zingesaidia kupata ufumbuzi wa tiba ya ugonjwa huo, kitu ambacho nchi maskini za Afrika hazina uwezo wa kuwekeza kwenye tafiti hizo.
Aidha, Annan ameonekana kuvunjwa moyo na jitihada zinazofanywa na mataifa makubwa ikiwemo Marekani kutangaza utaratibu mwisho wa wiki iliyopita wa kuwaweka karantini wauguzi na madaktari waliotoka Afrika Magharibi kwa siku 21, kitu ambacho kinarudisha nyuma ari ya wahudumu hao kujitolea kusaidia wagonjwa kwenye nchi zilizoathirika na Ebola.
Amesema njia pekee ya kuimaliza Ebola ni kufanya jitihada na mapambano ya pamoja katika kuzisaidia nchi za Afrika Magharibi na sio kwingineko, na kuongeza kuwa Afrika inachohitaji ni msaada wa vifaa, madawa na wauguzi ili kupambana na Ebola.
Mpaka sasa Liberia, Guinea na Sierra Leone zimetajwa kuathiriwa zaidi na Ebola, huku takwimu zikionesha zaidi ya watu 4,900 wamefariki na wngine zaidi ya 10,000 kupatwa na maambukizi ya ugonjwa huo

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako