A

A

WAATHIRIKA WA MABOMU MBAGALA KUU WAIBUKA WAMLILIA RAIS KIKWETE WAPATE MALIPO YA FIDIA STAHIKI


 WAATHIRIKA wa milipuko ya mabomu iliyotokea katika Ghala la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Mbagala Aprili 29 mwaka 2009 wameibuka upya wakimuomba Rais Jakaya Kikwete kuwasaidia wapate malipo stahiki kutokana na milipuko hiyo iliyosababisha vifo na kuharibu nyumba na mali zao mbalimbali. 

Ombi hilo limetolewa na waathirika hao kupitia Mwenyekiti wao Steven Gimonge katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na waathirika hao zaidi ya 300 uliofanyika leo asubuhi viwanja vya Shule ya Msingi Mbagaala Kuu iliyopo Manispaa ya Temeke. 

Alisema kwa muda mrefu waathirika hao wamekuwa wakiidai serikali iwalipe fidia tangu uharibifu ulipotokea ambapo serikali ilikubali ingawa fidia waliyolipwa awali haikulingana na uharibifu uliowapata. 

 Gimonge alisema pamoja na fidia hiyo ndogo walipewa fursa ya kuandika barua za mapunjo ambapo kwa mara kadhaa walilipwa fidia ndogo ambapo aslitolea mfano mtu kulipwa fidia ya sh.1400, 2700, 1950 na 4900 mpaka Machi 12 mwaka jana kufikia uamuzi wa kupanga maandamano ya kwenda Ikulu kumuona Rais Jakaya Kikwete. 

 Aliongeza kuwa wanapenda kumkumbusha Rais Jakaya Kikwete kuwa alipokwenda kuwafariji baada ya milipuko hiyo alitoa ahadi ya kuwapa kifuta machozi pamoja na kufidiwa na hata kijiko kilicho potea lakini hadi leo hii wamekuwa wakipigwa danadana. 

Katika hatua nyingine wamemlalamikia Mbunge wao Dk.Faustine Ndugulile kwa kuwaacha bila ya kuwasaidia wakati alionesha njia ya kulipekea suala hilo Bungeni lakini tangu afike huko amebadilika na hakuna mawasiliano yoyote jambo ambalo linawashangaza. 

 Waahtirika hao wanamuomba kwa mara nyingine Rais Kikwete awasaidia kupata fidia hiyo kwani ile iliyotolewa awali ilikuwa kidogo ukilinganisha na ukubwa wa kuathirika kwao.
 Mwenyekiti wa waathirika wa mabomu wa Mbagala Kuu, Steven Gimonge akionesha daftari lenye majina ya waathirika hao na jinsi malipo yalivyofanyika wakati akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi katika mkutano wa hadhara uliowahusisha waathirika wa mabomu hayo yaliyolipuka katika ghala la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Aprili 29,2009.
 Mwenyekiti wa waathirika wa mabomu wa Mbagala Kuu, Steven Gimonge, akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kulia ni Katibu wa Waathirika hao, Thomas Mbasha. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Waathirika hao hapa wakionesha mabango yenye ujumbe tofauti tofauti.
 Mmoja wa waathirika wa mabomu hayo akiwa amejiinamia kwa huzuni huku akitafakari kama Rais atawaonea kwa jicho la huruma wapate fedha hizo kulingana na ukubwa wa kuathirika kwao.
 Mabango zaidi yenye ujumbe tofauti yakioneshwa mbele za kamera za wanahabari.

 Waathirika hapo wakiwa kwenye mkutano huo kujadili jinsi serikali itakavyowapatia fedha zao kulingana na ukubwa wa kuathirika kwao baada ya malipo ya awali kudai walipunjwa.
 Waathirika hao wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Mbagala Kuu Dar es Salaam leo asubuhi.

 Baadhi ya wazee na vijana waathiriwa wa mabomu hayo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Waathirika wakisisitiza kulipwa malipo hayo ya ziada baada ya awali kudaiwa kutolewa kidogo.
 Mkazi wa Mbagala Kuu, Johanaina Mkukumbe akielezea jinsi walivyoa athiriwa na mabomu hayo pamoja na fidia kiduchu waliyolipwa.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako