A

A

Safu mpya ya uongozi CHADEMA




  1. Mwenyekiti: FREEMAN MBOWE
  2. Makamu Mwenyekiti Bara: Profesa ABDALLAH SAFARI
  3. Makamu Mwenyekiti Zanzibar: SAID ISSA MOHAMED
  4. Mwenyekiti wa Baraza la Wazee: HASHIM JUMA ISSA
  5. Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake: HALIMA JAMES MDEE
  6. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana: PASCHAL KATAMBI PATROBAS
Katika uchaguzi huo, Mbowe alipata kura 789 dhidi ya 20 za mpinzani wake. 
Prof. Safari ambaye hakuwa na mpinzania, alipata kura 775.
Said alipata kura 645 dhidi ya 163 za Hamad Yusuf aliyekuwa akiwania kiti hicho pia.

Katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili, Septemba 14, 2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, mgombea wa kiti cha Uenyekiti Taifa, Kansa Mohamed Mbaruku (Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA mkoa wa Tabora) alijitoa siku moja kabla ya uchaguzi kwa madai kuwa
katiba ya chama hicho imekiukwa hivyo akasema atakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uchaguzi huo na kuomba ufafanuzi wa kikomo cha uongozi.

Awali Mbaruku aliwasilisha pingamizi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, ambapo pamoja na mambo mengine, alidai kwamba Mbowe hana sifa kikatiba ya kugombea tena nafasi hiyo.
Pia duru za siasa ndani ya chama hicho zilieleza kwamba, majina mawili yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda katika chama hicho, Benson Kigaila, kwamba nao walijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti, Daniel Ruvanga na Garambenela Frank, yalikuwa majina hewa yaliyolenga kumsafishia njiaMbowe ya kubakia kuwa mgombea pekee baada ya kuenguliwa kwa Mbarouk.

Inaelezwa kwamba, Katiba ya Chadema hairuhusu kiongozi wa nafasi hiyo kugombea vipindi zaidi ya viwili vya miaka mitano.

HASHIM JUMA ISSAMwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA 

HALIMA JAMES MDEEMwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA - BAWACHA
PASCHAL KATAMBI PATROBAS Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA - BAVICHA
PASCHAL KATAMBI PATROBAS
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA - BAVICHA






CHADEMA founder, Mzee Edwin Mtei, greets party delegates and invitees to the opposition party’s General Meeting held at Mlimani City in Dar es Salaam. Left (partly hidden) is Secretary General, Dr Wilbroad Slaa, while second left is the National Chairman, Mr Freeman Mbowe. (Photo by Robert Okanda/The Daily News)
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akiwapungia mkono wajumbe wa mkutano mkuu.





No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako