A

A

Rihanna ampigia mikausho Chris Brown kwenye mechi ya basketball


0
Chris Brown na Rihanna wamejikuta wapo karibu kwa umbali mdogo sana walipokua kwenye mechi ya basketball kwa ajili ya kuchangia taasisi ya CC Sabathia na Robinson Cano. Mechi hiyo ilikuwa ya mafanikio kwa kuingiza zaidi ya dola milioni 1 lakini story kubwa sio hiyo.
Kitu kilichotengeneza headline ni pale Rihanna alivyoonyesha
mikausho mikali hasa wakati Chris Brown anapokuwa karibu yake wakati wa mechi hiyo. Kuna wakati Chris Brown alikuwa anawasalimia mashabiki waliokuwa wamekaa karibu na kiti cha Rihanna na picha zilipigwa Rihanna anaonekana ameweka mikausho na kuangalia pembeni.
Mechi iliisha vizuri na picha ya hapo juu imekuwa maarufu sana kwenye instagram hivi sasa.
1
2
3
4
5
6
7

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako