A

A

KUTOKA MAFINGA MCHANA WA LEO, CHADEMA WAFUKUZWA OFISI YA WILAYA WAKIDAIWA KUSHINDWA KULIPA KODI YA PANGO

 
MCHANA HUU BONGO LEAKS imepokea taarifa za kusikitisha kutoka wilaya ya Mufindi zikihusisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufukuzwa kutoka katika ofisi zake za wilaya zilizopo mjini Mafinga.
Taarifa za uhakika kutoka kwa mdau wa mtandao huu zimesema Chadema wamefukuzwa kutoka katika ofisi hiyo baada ya kushindwa kulipa kodi ya pango kwa kipindi kinachodaiwa kufika miezi nane.
Mdau huyo amesema mkataba ulikuwa unakita chama hicho kulipa Sh 80,000 kila mwezi na hivyo kufanya jumla ya fedha wanazodaiwa kufikia Sh 640,000.
Jengo ambalo Chadema walipanga liko upande wa pili wa stendi kuu ya Mafinga, karibu na kiwanda cha mbao likimilikiwa na mama aliyetajwa kwa jina la Mama Rachel.
Mpaka tunakwenda mitambani taarifa kutoka Mafinga zilikuwa zikionesha kwamba wafuasi wachache wa Chadema walijitokeza katika ofisi hiyo kuhamisha baadhi ya mali za chama hicho na kung’oa bendera yao.

Kama huo ndio ukweli, swali la kujiuliza hapa ni nani anayepaswa kulipa kodi za ofisi mbalimbali za chama hicho nchini?
Itaendelea……………….

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako