A

A

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA SADC NCHINI BOTSWANA,WIZARA YA FEDHA,VIWANDA NA UWEKEZAJI ZASHIRIKI.

Jopo la Uongozi wa Kikao hiki cha SADC hapa Botswana Phakalane Golf Estate Hotel.Mawaziri Kutoka Tanzania,Kuanzia kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba Naibu Waziri wa Fedha(S),Mh:Marry Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu na Mh:Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara wakijadiliana jambo kwenye Ukumbi wa mkutano wa SADC hapa Gaberone-Botswana.Sehemu ya ujumbe wa Mawaziri wa
Fedha,Biashara na Uwezeshaji kutoka Nchi mbalimbali za SADC wakiendelea na Majadiliano kuhusu Uwezeshaji wa Kifedha ndani ya Jumuia hiyo.
 Maamuzi na Majadialino ya Pamoja yakiendelea kwa Wajumbe Watatu Kutoka Tanzania kwenye Kikao cha SADC hapa Gaberone.
Mkutano unaendeleaMh:Marry Nagu Waziri wa Uweshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri  Mkuu,akijadiliana jambo na Mh:Mwigulu Nchemba. Mkutano huu wa SADC Umekutanisha Wizara tatu tofauti,Wizara ya Fedha,Bishara na Uwekezaji.Agenda kubwa inayozungumziwa hapa ni Kuiwezesha Jumuia hii ya SADC Kifedha iwezekufanikisha baadhi ya miradi ya maendeleo katika Nchi wanachama.Pia Kuondoa Vizuizi kwaajili ya Kuruhusu Biashara huria.Hawa ni Wataalum kutoka Tanzania waliofika pamoja  na Mawaziri kwaajili ya mkutano huu wa SADC.Ujumbe kutoka Namibia ukifurahia jambo kwenye Mkutano huu wa SADC.Mwenyekiti wa mkutano huu akijadiliana jambo na katibu wake.

Gaberone-Botswana.
SADC imefanya mkutano wake uliojumuisha sekta tatu tofauti,Fedha,Biashara na Uwezeshaji nchini Botswana Mji wa Gaberone,Mkutano ulioanza Tar.11/07/2014 na kumalizika hii leo Tar.18/07/2014.
Tanzania katika mkutano huo imewakilishwa na Mawaziri kutoka Hazina(Mh:Mwigulu Nchemba),Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu Mh:Marry Nagu na Waziri wa viwanda na Biashara Mh:Abdallah Kigoda.Mkutano huu wa SADC Umejikita kwenye majadiliano ya kufikia makubaliano ya kuanziasha kwa biashara huria na kuondoa vikwanzo mf.Ushuruwa forodha n.k.(Boosting Inter-African Trade-BIAT).
Pia kuanzishwa kwa mfuko wa kifedha utakaowezesha jumuia ya SADC kuendesha miradi yake ya maendeleo kwa ufanisi katika Nchi wanachama wake.Agenda ya kuanzishwa kwa mfuko wa kifedha ilianza kujadiliwa kwenye kikao cha SADC Kilichofanyika Maputo-Mozambique mwaka 2012 na 2013.
Picha/Maelezo na Festo Sanga
Gaberone-Botswana.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako