A

A

LOWASSA:AVEVA USILIPIZE KISASI

lowassa8july_dfd12.jpg
WAZIRI Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ameutaka uongozi mpya wa Klabu ya Simba kutolipiza kisasi au kufukua maovu ya uongozi uliopita na badala yake kujikita katika kuweka mikakati ya kuendeleza klabu.
Lowassa alisema hayo ofisini kwake Dar es Salaam jana alipotembelewa na Rais mpya wa Simba, Evans Aveva. Lowassa amemtaka Aveva kuunganisha wanachama wa Simba kwa manufaa ya soka la Tanzania
Aidha, aliwataka viongozi wa klabu kubwa nchini kusajili zaidi wachezaji wa nyumbani na kuachana na tabia ya kukimbilia kusajili wachezaji wa kigeni kwani hiyo inadhoofisha uimara wa timu ya taifa.
Lowassa alitolea mfano timu ya Taifa ya England ilivyofanya vibaya katika fainali za Kombe la Dunia la Fifa akisema inatokana na klabu za Ligi Kuu ya nchi hiyo kuwa na wachezaji wengi wa kigeni kuliko wa ndani.
Kwa upande wake, Rais huyo wa Simba, Aveva alisema uongozi wake umejipanga kuwekeza katika vijana ili kupunguza gharama za kusajili wachezaji wapya kila msimu.
Pia alimweleza Lowassa kuwa wanatarajia kufungua hosteli katika kipindi kifupi kijacho katika eneo jipya la klabu hiyo Bunju katika Manispaa ya Kinondoni.
Amesema awamu ya pili ndiyo itakuwa ya ujenzi wa uwanja ambapo alimwomba Lowassa kukubali mwaliko wa kufanya harambee ya kukusanya fedha za ujenzi wa uwanja huo wakati ukifika.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako