Mtanzania huyu hakufahamika Jina akielekea Kwenye Sherehe za Nyama Choma na Michezo Mwendelezo wa Miaka 50 ya Muungano Wa Tanzania.
Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na Balozi Mulamula wakati wa Michezo na Nyama Choma zinaendelea Kufana hapa Washington DC.
Watoto Wakiburudika katika Mchezo wa Bembea walipofika Kwenye Mkusanyiko wa Watanzania Kwenye tamasha la Michezo na Nyama Choma hapa Washington DC.
Nyama Choma Imepamba Moto,Wadau wakibeba Sufuria Kuelekea eneo la tukio.Nyama inaendelea Kuchomwa na Sausage.
Nyama choma ya Bure na Vinywaji ni
Buree.
Watanzania wakiendelea Kutafuna Nyama kwenye Tamasha la Michezo na Nyama Choma hapa Washington DC kwa Watanzania.
Mwandishi wa Habari Kutoka Kwanza production akifanya Mahojiano na Mh:Mwigulu Nchemba kuhusu Bunge la katiba,Maadhimisho ya Miaka 50 na Tamasha la Nyama Choma kwa Watanzania hapa Washington DC.
Watanzania na Nyama Choma Kama Samaki na Maji,Wadau wakipata Nyama choma.
Wanafamilia wa Tanzania hapa Washington wakiwasili Kwenye Nyama Choma na Tamasha la Michezo.
Nyama Choma Is All about.Watoto wa Kike pia walikuwa na nafasi ya Kuonesha Uwezo wao kwenye Soka.
Mh:Mwigulu Nchemba na Balozi Libereta Mulamula Wakielekea Kufungua Tamasha la Michezo,Mpira wa Miguu na Michezo Mingine hapa Washington.
Tanzania Bara Vs Tanzania Visiwani(Kilimanjaro Starz Vs Zanzibar Starz).
Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wachezaji wa Kilimanjaro Stars kabla ya Kuanza Mpambano wa Mechi ya Kirafiki ya Kudumisha Muungano Wetu.
Bi.Loveness Mamuya "IRON LADY" Shabiki Mtiifu wa Kilimanjaro Stars akisalimiana na Mh:Mwigulu Nchemba kabla ya Mechi ya Mpira wa Miguu Kuanza.
Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wachezaji wa Zanzibar Heroes kabla ya Kuanza kwa Mchezo.
Mh:Mwigulu Nchemba katika picha ya Pamoja na Kikosi cha Zanzibar Heroes.
Mh:Mwigulu Nchemba katika Picha ya pamoja na timu ya Kilimanjaro Stars hapa Washington DC.
Wimbo wa Taifa Unaimbwa,Wachezaji wameweka Mikono yao Sawa Kuheshimu Wimbo.
Hili ndilo Kombe atakalo Kabidhiwa Mshindi wa Mechi kali ya Mpira wa Miguu kati ya Kilimanjaro Stars VS Zanzibar Heroes.
Winga wa Zanzibar Heroes akimiliki Mpira kuelekea kwenye Lango la Kilimanjaro Stars.
Wachezaji wakioneshana Uwezo.
Mfungaji wa Kilimanjaro Stars akijaribu Kumimina Majaro kuelekea Lango la Zanzibar Heroes,Shuti lake halikuwa na Madhara.
Winga Namba 7 wa Kilimanjaro Stars akimiliki Mpira kueleka Lango la Zanzibar Heroes.
Shambulizi Kali Langoni kwa timu ya Zanzibar Heroes.
Mpambano Mkali Unaendelea.Zanzibar Heroes wakishambilia Langoni wa Kilimanjaro Stars.
Wachezaji wa timu Zote Mbili wakizozana Mara baada ya Zanzibar Heroes kupata Penati,Penati ilipigwa Kiufundi na Zanzibar wakapata Goli.
Mashabiki wa Kilimanjaro Stars wakipata UKODAK.
Tamasha la Michezo limefana sana,Watanzania wamejitokeza kwa Wingi na Familia Zao.
Watanzania Wakifurahia Moja ya Tukio la Kuvuta kamba lililokuwa lianendelea Uwanjani.
Mr& Mrs Loveness Mamuya.Watanzania wakibadilishana Mawazo kwenye Tamasha la Michezo lililojumuisha Watanzania hapa Washington DC.
Mh:Mwigulu Nchemba akifurahia na Mke wake Kipenzi Bi.Neema Nchemba.Watoto wa Kitanzania Wakifurahia Jambo.
Balozi Mwinyi akipata Ukodak na Miss Temeke wa Kwetu Fashion.
Mpira Unaendelea na Kufaidi Nyama Choma Kuanaendelea Nje ya uwanja.
Wadau Wakipata UKODAK.
Wadau wakipumzika wakati Michezo inaendelea.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Washington ambaye sasa ni Katibu wa Jumuia ya Wana-DMV Ndugu Amosi Cherehani.
Katika hali ya Kuonesha Mshikamano na Umoja wa Watanzania hususani hapa Marekani,Hii leo tar 27/04/2014 Watanzania wamekutana tena Kwenye Tamasha la Michezo na Nyama Choma kwa Lengo la Kuimarisha Umoja na Muungano wetu uliochini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tamasha limefana sana na Watanzania wamejitokeza kwa WIngi Kutoka Majimbo mbalimbali hapa Marekani wamefika Washington Kujumuika pamoja,Ni tukio la aina yake ambalo Watanzania na Familia zao wameweza Kujamiiana na Kufahamiana Vizuri mbali na Maisha yao ya Kila siku hapa Marekani.
Katika Mchezo wa Mpira wa Miguu,Mchezo umemalizika kwa sare ya Magoli 2 kwa 2 ambapo Kilimanjaro Stars walifanikiwa Kupata Magoli yote mawili kipindi cha Kwanza na Baada ya Mapumziko Zanzibar Heroes wakafanikiwa Kurudisha Magoli yote Mawili hali ilioleta msisimko Mkubwa sana kwa Mashabiki hasa Ukizingatia Kipindi hiki Watanzania wanapigania Serikali mbili ziendelee Kuwa nguzo za Muungano wa Tanzania,Hivyo Magoli Mawili kwa kila Upande wa Muungano yaweza Kutafsiriwa kuwa ni Kuunga Mfumo wa Serikali mbili(Ni Mawazo Binafsi)
Mwisho wa Mchezo timu zote Mbili zilifanya Maridhiano ya Kila timu Iinue Kombe na Kushangilia na baadae Kumkabishi Balozi Libereta Mulamula.
Picha/Maelezo na Festo Sanga-Washington DC.