A

A

LULU AOGESHWA POMBE UKUMBINI... AANGUA KILIO KAMA MTOTO


Kha! Katika hali isiyoitarajiwa, nyota wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ amejikuta akiangua kilio cha ukweli kama mtoto kufuatia kuogeshwa kwa pombe mwilini, jambo ambalo hakulitarajia. Nyota wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akimwagiwa pombe kwenye birthday yake.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Aprili 16, mwaka huu ndani ya Hoteli ya Regency, Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo
                                                               Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya lulu
marafiki wa Lulu wasio mastaa walimwangushia ‘sapraizi’ ya nguvu ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa (bethidei). Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kilizama ndani ya sherehe hiyo bila waalikwa wote kujua kuwa ni ‘shushushu’ wa
kujitegemea, Lulu aliitwa kwenye sherehe hiyo akiwa hajui kitu japokuwa akilini mwake alitambua kuwa siku hiyo ni bethidei
yake.
TAARIFA YA AWALI
Awali, Risasi Jumamosi lilitonywa na mtonyaji wake wa habari za mastaa wa Bongo kwamba, Lulu siku hiyo anafanya bethidei ya

nguvu maeneo ya Mikocheni lakini eneo sahihi likiwa halijulikani.
“Jamani nawapa habari ya mjini kama kawaida yangu. Leo (Jumatano), Lulu anafanya bethidei. Nasikia ni Mikocheni, nimejaribu

kupeleleza ni sehemu gani nimeshindwa, kwa sababu ninyi ni wadaku hebu jiongezeni mpeleleze wenyewe,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza: “Lakini nahisi kuna mazingira ya usiri. Hakuna staa hata mmoja atakayekuwepo kwa sababu sherehe yenyewe

imeandaliwa na marafiki zake wa kawaida.”

LULU APIGIWA SIMU, AKIRI, AKWEPA    
Baada ya chanzo hicho kuachia taarifa hiyo nyeti, Risasi Jumamosi lilimsaka Lulu kwa njia ya simu yake ya mkononi.
Risasi Jumamosi: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, niambie.
Risasi Jumamosi: Poa. Tumesikia leo ni bethidei yako, ni kweli?
Lulu: Ni kweli ndiyo.
Risasi Jumamosi: Itafanyika wapi?
Lulu: Mikocheni.
Risasi Jumamosi: Mikocheni sehemu gani?
Lulu: We tambua tu ni Mikocheni, mi mwenyewe sijui ni sehemu gani ndiyo nataka kwenda. Kwanza nimefanyiwa sapraizi na
marafiki zangu.

BAADA YA KUPIGWA CHENGA NA LULU
Baada ya Lulu kukwepa kutaja eneo la tukio, ndipo timu ya Risasi Jumamosi ikawasiliana na kamanda wa kikosi maalum cha

Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kumpa kazi ya kujua bethidei ya Lulu itafanyika wapi katika jijini la Dar es Salaam siku
hiyo.
NDANI YA DAKIKA 45
Ndani ya dakika arobaini na tano, kamanda wa OFM alirejesha majibu kwamba, sherehe hiyo itafanyika kwenye Hoteli ya Regency

iliyopo Mikocheni, Dar lakini hakutakuwa na mastaa na inafanywa kuwa siri ili mapaparazi wasijue na kufika kupiga picha.

KILICHOTOKEA
Usiku uliingia, Risasi Jumamosi likatia timu kwenye eneo la hoteli hiyo ambapo lilibahatika kumpata mtu mmoja akiwa anaelekea

kwenye sherehe hiyo.
Katika mazungumzo yake na Risasi Jumamosi, mtu huyo (jina lipo) alisema kila kitakachotokea ndani ya shughuli hiyo atakiweka

wazi ili mradi asitajwe jina gazetini tu!

BAADA YA SHEREHE
Saa saba na nusu usiku, sosi wetu huyo alilipigia simu Risasi Jumamosi na kuweka wazi yaliyotokea kwenye bethidei hiyo.
Sosi: Jamani shughuli imekwisha.
Risasi Jumamosi: Nini kimetokea?
Sosi: Lulu aliogeshwa pombe hivihivi nikishuhudia. Mbaya zaidi wale waliomwogesha nahisi walikuwa wanafanya makusudi, maana

walikuwa wanammiminia kuanzia kichwani hadi miguuni, yaani mwili wote chapachapa.
Risasi Jumamosi: Mwenyewe alikuwa anasemaje?
Sosi: Kilio. Lulu Amelia sana. Siyo kwamba alikuwa analia utani, ukweliukweli. Si unajua yeye aliacha kunywa pombe tangu ule

mkasa wake na marehemu Steven Kanumba, sasa leo kuogeshwa pombe hiyohiyo mwili mzima, nadhani ndiyo maana amelia sana.

MAMA YAKE AMSHANGAA
“Ilibidi Lulu ampigie simu mama yake (Lucresia Karugila) na kumweleza yaliyomkuta, akajuta hata kuhudhuria. Mama alishangaa

lakini alimuuliza kama yupo salama akasema yupo salama,” alisema shushushu wetu.

LULU ABADILI NGUO
Sosi huyo aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya kuwa chapachapa kwa kulowa pombe, Lulu aliyetengenezewa keki tano,

alilazimika kwenda kuoga na kubadili nguo mara mbili. Mwisho alivaa gauni la rangi ya kahawia.
“Naamini alibadili hata nguo za ndani, maana alilowa pombe mwili mzima,” kilisema chanzo hicho huku kikisisitiza kwamba jina
lake liwekwe kapuni.

MASTAA WAKAUKA
Ilidaiwa kuwa tofauti na shughuli nyingine za mastaa ambapo mastaa wenzake hujaa, bethidei hiyo ya Lulu mtu mwenye jina kubwa

Bongo aliyehudhuria sherehe hiyo ni Mahsin Awadh ‘Dk. Cheni’ peke yake.

KWA MAANA HIYO
Kwa sherehe hiyo, Lulu ametimiza miaka 19 tangu kuzaliwa kwake. Alizaliwa Jumapili ya Aprili 16, 1995.
CHANZO GPL