A

A

Kwa Mara ya kwanza Rais Uhuru Kenyata Awasili Arusha akitokea Kenya


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta jana alisafiri kuelekea mkoani Arusha nchini Tanzania kwa usafiri gari kwa njia ya barabara, safari ya umbali wa kilometa 230.

Rais Kenyatta alisimama katika maeneo kadhaa kabla ya kuvuka mpaka wa Namanga kwa kutumia kitambulisho kipya kinachoruhusu wananchi wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia kusafiri baina ya nchi hizo kwa urahisi.

Akiwa Arusha, Rais Uhuru atazuru Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambako atapokelewa na
katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dk Richard Sezibera.
Siku ya Jumanne anatarajiwa kulihutubia bunge la Jumuiya hiyo kwa wadhifa wake wa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa sasa. Anatarajiwa kusisitiza mshikamano na ushirikiano baina ya nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.