Ndani ya wiki moja iliyopita Balozi wa Tanzania nchini China aliongea Exclusive na millardayo.com na kuthibitisha kwamba hajawahi kupokea taarifa kutoka gereza lolote la China juu ya kukamatwa na dawa za kulevya kwa Mtanzania, mrembo ambae amekua akitokea kwenye video kadhaa za bongofleva “Jackie Patrick Cliff’
Maelezo yake yalifanya kuwe na maswali zaidi manake kila mmoja alikua
anajiuliza atakua wapi Mtanzania huyu baada ya taarifa kusambaa kwenye
vyombo vya habari Tanzania kwamba kakamatwa huko Macao?
Boyfriend wake ambae ni msanii wa bongofleva Jux ameongea kwenye
Exclusive interview na millardayo.com Jan 13 2014 saa kadhaa baada ya
kuweka post ambayo ilionyesha wamewasiliana muda mfupi uliopita.
Baadhi ya maswali aliyoyajibu kwenye video hapa chini ni pamoja na
Wameongea lini mara ya mwisho? Jack anasemaje? Jack alikua wapi wakati
wanaongea? yuko nchi gani? anarudi lini bongo? na mengine…