A

A

BILIONEA MO DEWJI LEO APANDA BODABODA KUWAHI KIKAO KUTOKANA NA FOLENI JIJINI DSM




Mohammed-Dewji

Foleni Yasababisha Mh.Mohammed Dewji Kupanda Boda Boda …

Kwa jinsi inavyoonekana hapa jijini Dar-Es-Salaam, kila kukicha foleni kama inaongezeka na imekuwa ikileta kero sana kwa wakazi wa jiji hili ambapo mambo mengi huwa hayaendi kama inavyotakiwa kutokana na wakazi kushindwa kufika maeneo ya mipango yao katika muda muafaka. Na hii hali ya foleni ya jiji la Dar husababishwa na kuongezeka kwa magari mengi na pia kuwa na barabara finyu ambapo ikitokea hali ya mvua kidogo tu basi hali ndo inazidi kuwa mbaya.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter leo, Mheshimiwa na mfanyabiashara mkubwa jijini Dar Bw. Mohamed Dewji alitoa malalamiko yake katika akaunti yake ya twitter kuwa anahitaji kuwa na Helicopter ili aweze kuwahi na kuepuka foleni ya jiji la Dar. Na hii hapa chini ndiyo kauli aliyotoa Mheshimiwa huyo baada ya kulazimika kupanda usafiri aina ya Boda Boda ili asichelewe kufika katika mkutano ambao alitakiwa kuhudhuria …
mdj

1 comment:

Toa maoni yako lakini angalia kuchafua hali ya hewa na usimuumize mwenzako